Msafara wa Sanara
Jinsi Sanara inavyofanya kazi
Nguzo nne. Unaamua pa kuanzia.
Anza Popote ulipo
Njia ya ubunifu haina mstari mmoja wa kufuatwa, na Sanara haijajengwa kama mtaala wa lazima kufuatwa hatua kwa hatua. Unaweza kuanza kwa kupata ufadhili, kisha ukaendelea na mafunzo. Au ukaanza na warsha, kisha utume ombi la mkopo wakati biashara yako iko tayari. Nguzo hizi nne zinazofuata, zinapatikana kwa mpangilio wowote unaoendana na mahali ulipo kwa sasa.
Mafunzo Ya Ujuzi Kwa Ajili Ya Kazi
Mafunzo ya vitendo, sio nadharia
Baraza Media Lab inaratibu programu za mafunzo za Sanara, ikifanya kazi na washirika waliobobea katika kaunti zote sita. Lengo kuu likiwa ni kupata ujuzi unaohitajika wa soko la taaluma za ubunifu: upigaji picha wa sinema, ushonaji wa mavazi, mkakati wa maudhui ya kidijitali, utayarishaji wa sauti, uelewa wa biashara, na mengi mengineyo.
Vituo vya Sanara katika kila kaunti vinatoa fursa ambapo unaweza kupata vifaa, kuhudhuria warsha na kuungana na wabunifu wengine katika eneo lako la kazi.
Upatikanaji Wa Fedha
Mtaji unaolingana na mahitaji ya biashara za ubunifu
Bidhaa nyingi za ufadhili zimeundwa kwa kuzingatia jinsi biashara katika sekta nyingine zinavyofanya kazi. Ila bidhaa ya Ota ya HEVA Fund umeundwa kwa mtazamo tofauti, ikiwa na mifumo ya malipo inayozingatia uhalisia wa uzalishaji wa ubunifu — mapato yasiyo ya kawaida, mizunguko ya miradi na mapato ya misimu.
Bidhaa tatu zinapatikana kwa washiriki wa Sanara wanaostahiki.
- Ota Kopa (hadi KSh 999,999): Kwa mahitaji ya haraka ya uendeshaji wa biashara — vifaa, bidhaa za kuuza au mtiririko wa fedha.
- Ota Kopa+ (KSh milioni 1 hadi milioni 4.9): Kwa biashara zilizo tayari kukuza uzalishaji wao au kufikia masoko mapya.
- Ota Growth (hadi KSh milioni 20): Kwa biashara za ubunifu zilizoimarika zinazopania kupanua shughuli zake kitaifa au kimataifa.
Mikopo yote ya Ota ni bidhaa za HEVA Fund, inayotolewa kwa riba ya 9% kwa waombaji wanaokidhi vigezo.
Ukuzaji Ya Biashara
Mifumo inayofanya kazi ya ubunifu iwe endelevu
SNDBX-Ubuntu inaongoza nguzo hii, ikitoa usaidizi wa mahususi wa kibiashara kwa kazi za ubunifu. Hii inajumuisha ushauri elekezi wa ana kwa ana kutoka kwa wataalamu wa sekta, mafunzo ya usimamizi wa fedha, na usaidizi katika harakati za kubadilisha uendeshaji wa biashara bunifu kutoka kwenye mfumo usio rasmi hadi kuwa biashara iliyosajiliwa na inayoweza kupata huduma za kifedha kupitia benki.
Lengo kuu sio kubadilisha jinsi unavyofanya kazi. Ni kukupa mifumo ya kuendesha biashara yako kwa ufanisi zaidi.
