Maswali Yanayoulizwa Mara Kwa Mara
(FAQs)
Je, Sanara ni shule? Hapana. Sanara ni mradi, si taasisi ya kitaaluma. Mafunzo tunayotoa ni ya vitendo na yanayolenga soko, na hutolewa kupitia washirika waliobobea katika taaluma za ubunifu. Hakuna shahada wala masharti rasmi yanayohitajika – ni ujuzi unaoweza kuutumia.
Kwa nini hakuna malipo kwa washiriki? Sanara haitoi malipo kwa kushiriki katika mafunzo. Badala yake, tunatoa mafunzo yaliyogharamiwa kikamilifu na, kwa biashara zinazostahiki, ufadhili kupitia HEVA Fund. Mfumo huu umejengwa kwa minajili ya kufanya uwekezaji katika kazi yako.
Mnafanya kazi katika kaunti zipi? Nairobi, Mombasa, Kisumu, Nakuru, Kakamega na Turkana. Iwapo upo nje ya kaunti hizi, Tafadhali wasiliana nasi – Tutakupa ushauri hutajika na ikiwa hali hii itabadilika.
Sijui nipo katika sekta gani ya ubunifu. Ikiwa kazi yako iko katika mavazi, vifaa vya mitindo au huduma za urembo, uko katika Mitindo, Mavazi na Vifaa vya Mitindo. Ikiwa ni filamu, upigaji picha, podikasti au maudhui ya kidijitali, uko katika Filamu, Televisheni na Uundaji wa Maudhui. Ikiwa kazi yako ni muziki, maonyesho au matukio, uko katika Maonyesho ya Moja kwa Moja. Ikiwa kazi yako iko katika zaidi ya eneo moja, tuma ombi kwa eneo linalofaa zaidi na utupe maelezo zaidi katika ujumbe wako.
Endelea kupata Taarifa
Njia ya haraka ya kupata taarifa kuhusu fursa zilizo wazi, matukio na mengineyo ni kupitia kundi letu la WhatsApp. Changanua msimbo hapa chini au bonyeza kiungo ili kujiunga.
Wailiana Nasi
Wasiliana nasi
Una swali? Tumia fomu hapa chini au tutafute katika kituo cha Sanara kilicho katika kaunti yako.
